Waziri Ummy Mwalimu asema Wagonjwa335 wapandikizwa Figo



Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema tafiti zimebaini kuwa takribani Watanzania 5,800 mpaka 8,500 wanahitaji huduma za kusafisha damu (dialysis) au huduma za kupandikizwa figo.

Waziri Ummy amesema hayo Jijini Dar es Salaam wakati akiongea na Waandishi wa habari akiwa jengo la Wagonjwa wanaosafishwa figo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo amesema hadi kufikia January 31, 2023 Wagonjwa 3,250 walikuwa wanapatiwa huduma ya kusafishwa damu (dialysis) na Wagonjwa 335 wamepandikizwa figo.

“Kati ya waliopandikizwa figo Wagonjwa 103 wamepandikizwa nchini ambapo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imepandikiza wagonjwa 70 na Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma imepandikiza wagonjwa 33”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad