"BBC Yakunja Mkia": BBC Kumuomba Msamaha na Kumrejesha Kazini Mtangazaji Aliyesimamishwa Kazi




Shirika la habari la Uingereza la BBC linatarajiwa kumuomba msamaha hadharani na kumrejesha kazini matngazaji aliyesimamishwa kazi majuzi.


Gary Lineker ambaye ni mtangazaji wa michezo anatarajiwa kurejea hewani na kuendelea na kipindi chake cha Match of the Day , shirika la habari la Sky Sports limeripoti.

Lineker alikuwa kwenye mzozo baada ya kuegemea upande katika lugha aliyotumia kulinganisha mfumo mpya wa serikali kuhusu kuwapa makao raia wa kigeni wanaokimbilia nchini humo na ule wa taifa la Ujerumani katika miaka ya 1930.


BBC ilimtimua kazini hadi pale ambapo angeomba msamaha kwa maneno yake lakini akadinda huku pia watangazaji wenzake wakisimama naye bega kwa bega.



Ian Wright na Alan Shearer walijiondoa katika vipindi huvyo huku pia watangazaji wa vipindi vingine vya michezo wakijiondoa.

Imekuwa wikendi ngumu kwa BBC na vipidi vyake vya soka hususan Match of the Day mnamo Jumamosi ambacho kilikatwa dakika 20 kabla ya kukamilika kikikosa watangazaji.

Kipindi hicho kilikosa matangazo mechi ikiendelea, uchambuzi wa mechi zenyewe, mahojiano baada ya mechi na hata muziki wa kutangaza kipindi hicho.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad