UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kitakachowakuta wapinzani wao kwenye Kombe la Shirikisho Afrika US Monastir, Waarabu wa Tunisia hawataamini.
Timu hiyo inashiriki Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa hatua ya makundi inasaka pointi tatu ili kufikisha malengo ya kutinga hatua ya robo fainali ina pointi 7 kwenye kundi D baada ya kucheza mechi nne.
Wawakilishi hao wa kimataifa wanakibarua dhidi ya US Monastri mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Machi 19 ipo wazi walipoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa mabao 2-0.
Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe alisema kuwa wanatambua kazi kubwa wanayo dhidi ya Waarabu lakini watawafanyia jambo la kipekee ambalo hawataamini.
“Tuliwafuata wakatufunga unadhani kuna ambaye alipenda? Hakuna aliyefurahia matokeo yale sasa wanakuja Uwanja wa Mkapa kitakachowakuta hao Waarabu hawataamini kila kitu kinakwenda kwa mpangilio mkubwa na sasa wanakuja ili kutupa tiketi ya kutinga robo fainali Kombe la Shirikisho.
“Mchezo wenye hadhi ya fainali mchezo wa maamuzi na wachezaji wanatambua kwamba kila mmoja anahitaji ushindi, wajitokeze kwa wingi ili kushangilia na kutakuwa na aina tofauti ya ushangiliaji ili kuwapoteza wapinzani wetu,” alisema Kamwe.
Stori: Lunyamadzo Mlyuka