KLABU ya Yanga imefanikiwa kuondoka na alama tatu baada ya kuichapa timu ya Real Bamako kwa mabao 2-0, katika mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Yanga Sc ilianza kupata bao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wao raia wa DR Congo Fiston Kalala Mayele dakika nane ya mchezo na kuwapeleka Yanga kipindi cha kwanza wakiwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili Real Bamako walirudi kwa kasi kwani waliengeneza nafasi nyingi pasipo kuzitumia nafasi hizo ndipo Yanga Sc ikafanya mabadiliko ya wachezaji wake, mabadiliko ambayo yalizaa matunda kwani alitoka Tuisila Kisinda na kuingia Jesus Moloko ambaye aliweza kupachika bao la pili na kufanya matokeo kuwa 2-0