Zari Hassan "Gigy Money Zamani Alikuwa Mchafu Sana Kama Vile Haogi"

 


Mjasiriamali kutoka Uganda mwenye maskani yake Afrika Kusini, Zarinah Hassan 'Zari The Boss Lady' amesema, msanii wa Bongo Fleva Gift Stanford 'Gigy Money' alikuwa mchafu sana zamani lakini kwa sasa amebadilika.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zari amemtumia ujumbe (DM) Gigy kumpongeza huku akimueleza jinsi alivyokuwa zamani na sasa.


"Umekatiza kwenye fikra zangu leo. Yani wakati nina mimba ya Tiffah ulikuwa unaonekana mchafu. Kama vile hukuwa unaoga sijui kama unakaaga wapi? Baada ya miaka umesafisha muonekano wako, brand yako.


"Umekua msafi na boss, unaonekana kuwajibika zaidi na wa viwango. Visa vimepungua, kabla ulikua na visa vya staili ya wanaoishi ghetto. Sasa inaonekana kama unachagua visa vyako kwa umakini.


"Nimetaka kukuambia endelea kuwa boss Inakupendezea. Napenda kuona dada akionekana kufanya vizuri. Ni fikra zangu tu za hapa na pale. Hata hivyo sijakutoa makosa nimekusifia."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad