Zuchu, Khadija Kopa wamtelekeza mtoto wa Omar Kopa

 


Rehema John Musa akiongozana na mwanae Najma Omar Kopa amejitokeza hadharani baada ya majukumu ya malezi kwa mtoto wake kumuelemea peke yake ikiwa kuna ndugu wa mwanae ambao ni maarufu na wana uwezo wa kuwasaidia.


Bi Rehema Jonh amesema yeye ni mwanamke ambaye alizaa mtoto na Marehemu Omar Kopa lakini kwa bahati mbaya Omar Kopa alifariki dunia miezi mitatu tu baada ya binti yake kuzaliwa hivyo kukawa ugumu kwenye swala la malezi, amesema kwa muda mrefu amekuwa akihangaika peke yake kutafuta ada ya kumsomesha binti yake na kuna wakati alilazimika kuponda zege ili apate pesa ya kumsomesha binti yake, ingawa anajitahidi lakini yeye kama binadamu na singo mama kuna muda anakwama na anakosa msaada kabisa kama alivyo kwa kipindi hiki.


Akizungumza kwenye maiki za "Simulizi na Sauti" Bi Rehema amesema ndugu wa mwanae ambao ni kina Khadija Kopa na wanae akiwemo Zuchu, wanajua kabisa kama yeye ana mtoto wao lakini wamekuwa wakimsusia kila anapohitahi sapoti kutoka kwao, hata hivyo amesema hana kinyongo nao kwakuwa anajua nao ni binadamu wana majukumu mengine au laa!! hawana pesa, lakini wanatambua kabisa kama Najma ni binti yao wa damu.


Naye mtoto huyo ambaye yupo kidato cha tatu amesema kuhusu swala la darasani siyo tatizo kwake kwani amekuwa akiongoza kila mara pindi linapokuja swala la mitihani, amesema anajisikia uchungu kuona ni mama yake pekee anayehangaika kumsomesha ikiwa yupo bibi yake Khadija Kopa ambaye ni msanii maarufu na mwenye pesa za kuweza kumhudumia, lakini pia yupo shangazi yake Zuchu ambaye ni msanii mkubwa ila wamemtenga na wakati mwingine wanamkwepa kila anapojaribu kujisogeza au kujiweka karibu nao.


Binti Najma amesema ndoto yake kubwa ni kuja kuwa mwanamuziki msomi kimataifa kwani ana kipaji kikubwa ambapo akiwa kidato cha tatu tu tayari ameshatoa wimbo ambao unaitwa "Come back" ambao amemuimbia baba yake, anatamani kama baba yake angekuwepo angeishi kwa furaha na wangekuwa na maisha mazuri.


Mama yake amesema kwasasa anadaiwa ada ya mwanae huyo na wakati wowote binti yake anaweza kusimamishwa masomo maana amekwama na kuomba yeyote atakayeweza kumsaidia basi amsaidie ili binti yake aweze kufikia malengo na atimize ndoto zake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad