Waswahili waliwahi sema “ukipenda ua basi penda na boga lake” huu ni msemo pekee unaonijia kila nikifikiria penzi la mwanadada Zuchu kutoka WCB na ‘boss’ wake Diamond Platnumz.
“Najua wivu ndo mapenzi ila chunga usizidi” ni mstari ambao upo kwenye moja ya nyimbo za nyota Diamond Platnumz.
Ni kama mwamba huyo alimuimbia mpenzi wake wa sasa (Zuchu) bila hata yeye mwenyewe kujua.
Hivi karibuni tumemshuhudia Tanasha Donna ndani ya Jumba la kifahari la Diamond Platnumz (Hii wazungu wanaiita ‘Co-Parenting’), Ila kwetu hapa Tanzania utasikia waswahili wanakwambia “Wazazi hawaachani bwana”.
Tukiachana na Donna kutoka Kenya, yupo mwanamama Zari kutokea Uganda huyu naye ni mama wa watoto watano, wawili wakiwa wa Diamond.
Mara kadhaa tumeshuhudia Zari akija bongo kwa ajili ya kuwaleta watoto kwa baba yao.
Kama unaelewa mapenzi na wivu basi unaelewa ni kitu gani Zuchu anakivumilia kutoka kwa Diamond kila wazazi wenza hao wanapokuja nchini.
Je, wewe unaweza kuvaa viatu vya Zuchu?