Air Tanzania Yakiri Kupitia Changamoto

 


Shirika la Ndege Tanzania limesema linapitia changamoto za mabadiliko ya ratiba za ndege kutokana na uchache wa ndege zilizobaki, uliosababishwa na kuchelewa kwa upatikanaji wa injini mbadala za ndege zetu mbili (2) za Airbus A220-300 zenye matatizo ya injini.


Kwa mujibu wa Taarifa ya Shirika hilo iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano kwa umma na kuchapishwa kwenye ukurasa wa Twitter imesema Injini mbadala zinazotakiwa kutolewa na mtengenezaji zilitarajiwa kuwasili mwanzoni mwa mwezi Aprili 2023.


Taarifa hiyo imeeleza kuwa, “kutokana na changamoto hizi, tunalazimika kutoa huduma kwaratiba inayobanana sana ili kukidhi mahitaji makubwa ya wateja wetu na wakati tunashughulikia changamoto hizi kwa haraka, tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.”


“Wakati tunashughulikia changamoto hizi kwa haraka, tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza. Kampuni ya Ndege itaendelea kuhakikisha inatoa huduma bora ili kufikia matarajio ya wateja wetu,” imeeleza taarifa hiyo



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad