Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Simba Sc, Luis Jose Miquissone kwa sasa yuko nyumbani na anafanya mazoezi yake ya kibinafsi ili kuwa fiti hadi msimu ujao.
Kocha Mkuu wa Al Ahly, Marcel Koller aliweka wazi kuwa Luis hayuko katika mipango yake ya msimu ujao. Kambi yake inafahamu hali hii na sasa iko tayari kupata suluhisho bora zaidi.
Qatar SC na Al Batin wamefanya mbinu rasmi kumnasa winga huyo lakini yote inategemea Al Ahly ambao wanataka kumuuza Luis moja kwa moja lakini watakaribisha pia uhamisho wa mkopo.
Hakuna mawasiliano kutoka kwa klabu nyingine yoyote hasa barani Afrika kwa sasa. Luis alitoa ahadi kwa Simba kabla ya kuondoka siku moja, atarejea.
Miquissone aliondoka Simba mwishoni mwa msimu wa mwaka 2020/21 na kujiunga na miamba hao wa soka barani Afrika lakini kiwango chake kimekuwa cha kusuasua hivyo klabu hoyo imeamua imweke sokoni.