Hamisi BSS asimulia alivyolazwa nje kumpisha mwana na demu



Kwa vijana wa kiume yawezekana hili lisiwe jipya sana lakini unapoona linasimuliwa na msanii kama Hamisi wa BSS, linaifanya iwe habari.


Hamisi wa BSS amesimulia kisa hicho kuwa kiliwahi kumtokea miaka kadhaa iliyopita ambapo alijaribu kuondoka nyumbani kwao na kwenda kuishi geto na mwanaye mmoja ambaye hakumtaja jina.


"Daah ilikuwa noma sana, nilikuwa nishalala. Jamaa anakuja saa nane usiku ananiambia kaja na mtu wake, tunafanyaje? Nikalazimika kumpisha, akaniuliza kama nimemaindi nikamwambia hamna, kawaida," alisema.


Hamisi anasema ishu hiyo ilimfanya aamue kurudi nyumbani kwao akiendelea kujitafuta maana aliona kwamba maisha bado hayajawa sawa kuweza kupanga.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad