Anayekodisha bunduki kwa Tsh 100,000 anaswa

 


Uchunguzi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa, umefanikisha kumnasa mmoja wa wamiliki halali wa silaha anayetuhumiwa kujipatia fedha kutoka kwa magenge ya uhalifu kwa njia ya kuzikodisha.


Taarifa iliyotolewa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi imesema mtuhumiwa huyo (jina lake limehifadhiwa) alikamatwa April 3, mwaka huu majira ya Saa 11:30 katika eneo la Kihesa Kilimani, mjini Iringa.


Amesema mtuhumiwa ametajwa kukodisha silaha zake hizo aina Shortgun na Rifle pamoja na risasi zake kwa Sh 100,000 kila moja katika kila tukio la uhalifu, jambo ambalo ni kinyume na sheria na utaratibu wa matumizi ya silaha.


“Tunakamilisha upelelezi na wakati wowote kuanzia sasa tutamfikisha mahakamani kujibu tuhuma hizo,” alisema na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi lao kutoa taarifa za viashiria vya uhalifu katika maeneo yao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad