Apewa Figo na Dereva Uber Bure, Walikuwa Hata Hawajuani


Mwanaume mmoja kutokea Jimbo la New Jersey Nchini Marekani ambaye alikuwa anahitaji sana figo amepewa zawadi ya maisha baada ya Dereva wa Uber kutoa figo yake kwa ajili yake.

Bill Sumiel (71) alichukuliwa kutoka kituo cha kusafisha damu (Dialysis centre) huko Newark, Delaware Marekani October 30, 2021 na Tim Letts (33) ambaye alikuwa Dereva wa Uber na wawili hao kwa walianza mazungumzo wakiwa wanarudi nyumbani kwa Sumiel Mjini Salem, katika Jimbo la New Jersey, ambapo Bill alimwambia Dereva Uber kuwa alikuwa akihitaji sana kupandikizwa figo kwa zaidi ya miaka mitatu.

Baada ya mazungumzo yaliyochukua takriban dakika 30 ambapo Bill alimuelezea Tim kuhusu changamoto za figo anazozipitia, Dereva wa Uber Tim alimwambia kuwa aliamini kuwa ni Mungu ambaye alimuweka kwenye gari lake kwa makusudi na katika hali ya kustaajabisha Dereva huyo alijitolea figo yake moja kwa hiari na kumpatia abiria wake, Sumiel alipigwa na butwaa huku akitetemeka, hakuamini kile alichokuwa anakisikia.

Kwa bahati nzuri, upasuaji ulifanikiwa na mwili wa Bill Sumuel ulikubali figo ya Letts, takribani miaka miwili tangu kukutana na Letts tukio ambalo aliona kama ni la miujiza, Sumiel amesema anakaribia kurudi katika hali yake ya kawaida na anajiona kama Mtu mwenye bahati sana kwa kupewa nafasi ya pili kwenye maisha na wamepanga kuwa Marafiki milele.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad