Apoteza Maisha kwa Kung’atwa na Kunguni Jela



Wakili wa familia Michael D Harper alitoa picha zinazoonyesha mwili wa Bw Thompson ukiwa umejaa kunguni. Anatoa wito wa uchunguzi wa uhalifu aliwaambia waandishi wa habari kesi inafunguliwa.

“Bw Thompson alipatikana akiwa amefariki katika seli chafu ya jela baada ya kuliwa akiwa hai na kunguni,” Bw Harper alisema kwenye taarifa.

“Jela alilowekwa Bw Thompson halikufaa hata kwa mnyama mgonjwa. Hakustahili kutendewa hili.”

Kulingana na ripoti ya Mkaguzi wa Matibabu wa Kaunti ya Fulton, Bw Thompson alipatikana akiwa hana fahamu akiwa jela mnamo 19 Septemba – miezi mitatu baada ya kukamatwa – na kutangazwa kuwa amekufa kufuatia majaribio ya polisi wa eneo hilo na wafanyikazi wa matibabu kutaka kumuamsha, kulingana na USA Today.

Bw Harper anasema rekodi za jela zinaonyesha maafisa wa kizuizini na wafanyikazi wa matibabu waligundua kuwa Bw Thompson alikuwa akidhoofika lakini hawakufanya chochote kutoa msaada au kumsaidia vinginevyo, iliripoti CBS News.

Ripoti ya mchunguzi wa matibabu ilisema kulikuwa na “uvamizi mkali wa kunguni” katika seli yake katika wodi ya wagonjwa wa akili lakini akaongeza hakuna dalili za wazi za kuonyesha kwamba alipata mfadhaiko wa akili kwenye mwili wa Bw Thompson.

Ripoti hiyo iliorodhesha chanzo cha kifo hicho kuwa hakijabainika.


Picha zilizotolewa na wakili huyo zinatoa picha mbaya ya Bw Thompson, ambaye uso na kiwiliwili chake vinaweza kuonekana vikiwa vimefunikwa na wadudu.

Mazingira ya jela kama inavyoonekana kwenye picha ni “ya kutisha”, alisema Michael Potter, mtaalamu wa wadudu katika Chuo Kikuu cha Kentucky, ambaye ni mtaalamu wa kunguni.

“Nimeshughulika na kunguni kwa miaka 20 na zaidi,” Bw Potter alisema. “Sijawahi kuona chochote kwa kiwango hiki ikiwa kwa kweli hii ndio hali ninayoona.”

Kuumwa na kunguni kwa kawaida sio kwa kusababisha kifo, lakini katika baadhi ya matukio nadra, Bw Potter alisema, kuwa katika mazingira ya mrundiko wa kunguni kwa muda mrefu wakiwa wanakushambulia kunaweza kusababisha upungufu wa damu mwilini yaani anemia kali, ambayo inaweza kuwa mbaya ikiwa haitatibiwa.

“Bed bugs feed on blood and very large numbers of bed bugs feed on very large amounts of blood,” Mr Potter said. In other extreme cases, Mr Potter said, victims may experience an allergic reaction and go into anaphylactic shock, which can also be deadly.

“Kunguni hula damu na idadi kubwa sana ya kunguni hula kiasi kikubwa sana cha damu,” Bw Potter alisema.

Katika hali nyingine mbaya, Bw Potter alisema, waathiriwa wanaweza kupata athari ya mzio na mshtuko wa anaphylactic, ambao unaweza pia kuwa mbaya sana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad