Web

Aziz Ki Aandaliwa Kuimaliza Geita Gold Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho



BAADA ya kuukosa mchezo wa jana Jumapili dhidi ya TP Mazembe kutokana na changamoto za usafiri, imefichuka kuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki sasa amepewa programu maalum ya kuhakikisha anakuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports dhidi ya Geita Gold.

Yanga jana Jumapili walikuwa wageni wa TP Mazembe katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa nchini DR Congo, huku Aziz Ki akiwa miongoni mwa wachezaji walioukosa mchezo huo wa kukamilisha ratiba kwani tayari Yanga walikuwa wamefuzu Robo fainali.



Jumamosi hii Yanga wanatarajiwa kuwa wenyeji wa Geita Gold katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports ambao unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Meneja wa Yanga, Walter Harrison alisema: “Aziz Ki alikosekana kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe kwa sababu za changamoto za usafiri lakini alipewa program maalumu za mazoezi kuhakikisha anakuwa fiti kuelekea mchezo dhidi ya Geita Gold.

“Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu wote tunakumbuka mchezo wa mwisho dhidi ya Geita Gold ulivyokuwa na ushindani na sasa tuna vita nyingine ya robo fainali nasi kama mabingwa watetezi ni lazima thakikishe tunashinda na kwenda hatua inayofuata.”

Stori na Joel Thomas

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad