Baba mkwe wa DJ Brownskin avunja kimya kuhusiana na video ya binti yake akinywa sumu


Baba mkwe wa DJ Brownskin ameongea baada ya ufichuzi wa hivi punde kwamba DJ Brownskin alimrekodi mkewe akinywa sumu.

Simon Mwangi ,ambaye ni babake marehemu Sharon Njeri, aliyekuwa mke wa DJ Brownskin alisema kuwa hakufahamu ugomvi wowote uliokuwa ukiendelea baina ya Brownskin na mke wake.


Alisema kuwa anachojua ni kuwa mwanawe alikunywa sumu na alipata habari ya kifo chake alipokuwa kazini. Mwangi alilalamika kuwa amekumbana na matukio haya mapya  kwenye mitandao ya kijamii kabla ya kupona  kwa kumpoteza binti yake.

Mzee Mwangi aliongeza kusema ataridhika tu haki ya marehemu bintiye ikipatikana.  Alisema haikuwa vizuri kwa Brownskin kuchukua video ya mke wake akinywa sumu.

"Huwezi chukua video ya mtu ambaye mmezaa naye watoto akifa ...alikufa kwa sababu alikuwa anakupenda ilhali wewe unamchukua video akifa, hiyo ndiyo zawadi waweza kumpa?" alisema Simon.


Mwangi alisema Brownskin alikuwa na nafasi ya kumpeleka mkewe hospitalini badala ya kumwacha afe.

Sharon Njeri aliaga mwaka uliopita baada ya kunywa sumu iliyomwangamiza.

Hivi majuzi, video iliibuka mtandaoni Njeri akionekana akinywa sumu hiyo.

 Jambo hilo lilizua hisia mseto huku watu wengi wakigadhabishwa na kumnyooshea kidole  DJ Brownskin wakidai kuwa lilikuwa ni tendo la kukosa ubinadamu kwa kuchukua video hiyo badala ya kuokoa maisha yake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad