Bangala aifunika Rivers, thamani yake inanunua kikosi kizima




ACHANA na maisha ya kifahari ambayo Yanga inaishi jijini Uyo ambako leo itacheza dhidi ya Rivers United, wawakilishi hao wa Tanzania wameonyesha jeuri nyingine mbele ya wapinzani wao kwa kuwa na mchezaji ambaye thamani yake inaweza kununua kikosi chote cha Rivers United.
Nyota huyo wa Yanga ambaye thamani yake inazidi kikosi chote cha Rivers ni kiungo wa ulinzi kutoka DR Congo ambaye thamani yake sokoni kwa sasa inazidi ile ya wapinzani wao na chenji ikabakia.
Kwa mujibu wa mtandao wa www.transfermarkt.com, thamani ya kikosi chote cha Rivers United kwa sasa ni Euro 225,000 (Sh 587 milioni), kiasi ambacho ni pungufu ya thamani ya Bangala kwa sasa kwa kiasi cha Sh 391 milioni.
Thamani ya Bangala kwa mujibu wa mtandao huo ni kiasi cha Euro 375,000 (Sh 978 milioni) ingawa inaweza kupanda au kushuka muda wowote kutokana na kiwango cha mchezaji husika kwa wakati huo pamoja na urefu na thamani ya mkataba wake.
Kufuru zaidi ipo kwa thamani ya kikosi kizima cha Yanga ambayo kwa mujibu wa mtandao huo unaofanya uchambuzi wa thamani za wachezaji, kinaweza kuwa mara 10 zaidi ya kile cha Rivers United kwa maana hiyo, kikosi kimoja cha wawakilishi hao wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Afrika inaweza kununua vikosi takribani 10 vya Rivers United.
Yanga kwa mujibu wa www.transfermarkt.com kikosi chake cha sasa kina thamani ya Euro 2.15 milioni ambazo ni sawa na Sh 5.6 bilioni.
Nyuma ya Yannick Bangala, yupo Joyce Lomalisa ambaye mtandao huo umeonyesha kuwa anashika nafasi ya pili kwa kuwa na thamani kubwa kwenye kikosi cha Yanga hivi sasa ambayo ni ya Euro 300,000 (Sh 782 milioni), kiasi ambacho bado pia kinazidi thamani ya kikosi kizima cha Rivers United inayovaana na Yanga leo jioni.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad