Bernard Morrison Kuivaa Simba SC April 16



Baada ya kukamilisha mpango wa kuongoza Kundi D, Kombe la Shirikisho Barani Afrika kwa kuichapa TP Mazembe 1-0, Benchi la Ufundi la Young Africans limeanza mapema kusuka mipango ya kuicheza Kariakoo Derby itakayopigwa Aprili 16 kuanzia saa 11:00 jioni katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es salaam.


Moja na mikakati hiyo ni kumuandalia programu maalumu kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Bernard Morrison ‘BM33’, ili awe fiti kuikabili Simba SC kwenye pambano hilo litakalokuwa la 110 tangu Ligi ya Bara ilipoasisiwa mwaka 1965.


Young Africans ilimwacha Morrison, jijini Dar es Salaam makusudi ili aendelee na programu maalumu ya kumfanya awe fiti zaidi baada ya kupona jeraha lake la nyonga lililomweka nje kwa zaidi ya mwezi, lakini imefahammika kuwa mpango huo ni mkakati wa Benchi la Ufundi ili kumtumia kwenye michezo miwili ijayo ya Young Africans pamoja na ile na Kariakoo Derby.



Taarifa zinaeleza kuwa Benchi la Ufundi la Young Africans chini ya Kocha Nasreddine Nabi aliyeko Ubelgiji akifuatilia hati ya kusafiria, limemwandaa kiaina Morrison kuivaa Simba SC kutoka na uzoefu na Derby huku akipewa mchezo wa Kombe la ASFC dhidi ya Geita Gold utakaopigwa Jumamosi (April 08) kisha ya Ligi dhidi ya Kagera ni April 11, mwaka huu.


“Kocha mkuu ndiye alipendekeza tusisafiri naye kuja DRC kwa sababu ana mpango naye. Anataka amtumie katika michezo miwili ijayo, ili apate utimamu wa mchezo ‘Game Fitness’ na kama ataonekana kuwa tayari basi huenda akaanza naye rasmi dhidi ya Simba SC kwani anaamini ni aina ya wachezaji wanayoiwezea michezo ya Dabi,” imeeleza taarifa hizo



Hata hivyo, Kocha Nabi amesema anamsikilizia Morrison awe fiti kwa kiwango atakachoridhika na baada ya hapo ataanza kumtumia.


“Morrison aliumia na alipopona akatukuta tupo kwenye michezo ya CAF iliyohitaji wachezaji walio fiti kwa asilimia zote, hiyo ndio sababu kuu hatujamtumia ila siku si nyingi mtamwona,” aliwahi kusema Nabi.


Morrison kwa msimu huu hadi sasa ameichezea Young Africans michezo 10 tu za Ligi na kufunga mabao mawili na asisti tatu, huku ile ya kimataifa akicheza miwili tu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad