#BREAKING: Sabaya aachiwa huru

 


Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya, ameachiwa huru leo Jumatano, Aprili 5, 2023 na Mahakama ya Hakimu mkazi Moshi baada ya kufutiwa mashtaka saba yaliyokuwa yakimkabili, ikiwemo uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka na kuongoza genge la uhalifu.


Sabaya alifikishwa tena katika Mahakama hiyo kwa ajili ya kusikiliza kesi ya Uhujumu uchumi namba 2/2022 iiliyokuwa ikimkabili.


Upande wa mashtaka umeeleza nia ya kuondoa mashtaka kufuatia majadiliano baina ya mshtakiwa na upande wa mashtaka ambapo umefikia kukubaliana kisheria.


Makubalianao hayo yamewasilishwa mahakamani hapo kama moja ya vielelezo muhimu vya kesi hiyo, huku mashtaka mengine mapya mawili yakitarajiwa kufunguliwa mahakamani hapo dhidi yake.


Msingi wa kesi hiyo iliyokuwa na mashtaka Saba alidaiwa Sabaya na wenzake wanne walijipatia kitita cha Sh milioni 30 kutoka kwa mfanyabiashara Alex Swai Wakimtisha kutoa taarifa zake za ukwepaji Kodi.




Tangu kesi hiyo ifunguliwe Juni 1, 2022 haikuwai kusikilizwa kutokana na sababu mbalimbali za kisheria lakini Septemba 7, 2022 washirika wanne wa Sabaya waliachiwa huru kwa makubaliano ya nje ya Mahakama na mwendesha mashtaka Mkuu wa serikali.


Washirika hao waliokuwa watuhumiwa katika kesi hiyo ni pamoja na Sylvester Nyegu, Nathan Msuya, John Aweyo na Antero Asey ambao Mahakama iliwakuta na hatia na kutakiwa kutoa faini ya Sh 50,000 na fidia ya Sh milioni 1 kwa Muathirika wa tukio hilo ambaye ni Alex Swai.


Ikumbukwe pia kuwa, Mei 2022, Mahakama Kuu ya Kanda ya Arusha ilimwachia huru Sabaya na wenzake wawili waliokata rufaa ya kupinga kuhukumiwa miaka 30 jela katika kesi ya unyangányi wa kutumia silaha.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad