CCM Yaitaka Serikali Kuwachukulia Hatua Waliotajwa Kwenye Ripoti Ya CAG,Takukuru Kufuja Mali Za Umma

CCM Yaitaka Serikali Kuwachukulia Hatua Waliotajwa Kwenye Ripoti Ya CAG,Takukuru Kufuja Mali Za Umma


Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa -Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani).

Chama tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Serikali kuwachukulia hatua kwa waliohusika kwenye ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka katika taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2021/22 na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).


Chama hicho kimetoa wito huo Jumamosi, Aprili 1, 2023 mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati kuu ya chama hicho, kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan.


Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Sophia Mjema amesema kamati kuu imesikitishwa na kuwepo baadhi ya maeneo mengine ambayo bado yanatakiwa kufanyiwa kazi ili kuondoa upungufu, udhaifu uliobainishwa, ikiwa ni pamoja na mifumo ya malipo na ukusanyaji wa mapato kutokusomana.



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad