CHADEMA: Kumuondoa bosi TGFA haitoshi.



Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia kwa Katibu Mkuu wake John Mnyika leo April 10,2023 wamechambua ripoti ya CAG ambapo pamoja na mambo mengine wamesema hatua za Rais wa Tanzania Dkt. Samia kutengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), Mhandisi John Nzulule pekee haitoshi bali hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa.


Akiongea na Waandishi wa Habari, Dar es salaam leo Mnyika amenukuliwa akisema “Ikulu wamezungumzia kutenguliwa kwa uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Wakala wa Ndege za Serikali(TGFA), ni vizuri Umma ukafahamu kwamba mzizi wa matatizo yaliyopelekea kuondokewa kwa Mkurugenzi huyu ni ununuzi wa Ndege za Serikali ambazo zimewekwa na kutumika na Kampuni ya ATCL”


“Lazima tutazame mchakato wa ununuzi wa Ndege hizi na pia hasara ya uendeshaji wa ATCL, hatua ya kumuondoa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege pekee yake haijitoshelezi, ni hatua inayolenga kufunika kombe, nitoe wito kwa Rais na Serikali kuchukua hatua kwa kuweka bayana madai yote ya ufisadi na hasara ya uendeshaji wa ATCL na kuchukua kwa Mawaziri na Makatibu Wakuu waliohusika na mchakato huu”


“Kwenye jambo hili vilevile hatua zilizoelezwa na Ikulu jana hatujaridhika nazo na tunahitaji hatua zaidi”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad