Siku kadhaa zilizopita, kiongozi wa Wabudha, Dalai Lama ali-make headline baada ya kusambaa kwa video inayomuonesha akimfanyia mtoto wa kiume vitendo vilivyotafsiriwa kuwa ni kinyume cha maadili.
Katika video hiyo, Dalai Lama alionekana akimbusu mtoto wa kiume kwenye shavu, kisha akambusu tena mdomoni na baadaye akamwambia amnyonye ulimi wake, jambo lililozua gumzo kubwa duniani kote.
Baada ya kelele kuwa nyingi duniani kote, hatimaye leo, April 10, 2023 kiongozi huyo amejitokeza hadharani na kuomba radhi kutokana na kitendo hicho.
Kupitia akaunti za mitandao ya kijamii na tovuti rasmi ya ofisi yake, Dalai Lama ameomba radhi katika ujumbe unaosomeka:
“Kumekuwa na kipande cha video kinachosambaa, kikimuonesha mvulana mdogo aliyekutana na kiongozi wetu, Dalai Lama na kumuomba amkumbatie.
“Kiongozi wetu anaomba radhi kwa mvulana huyo, familia yake pamoja na marafiki zake duniani kote kwa maumivu yaliyosababishwa na maneno yake.
“Ni kawaida kwa kiongozi wetu kufanya masihara kwa namna ya kucheza na watu anaokutana nao, hata mbele ya kamera. Kiongozi wetu anajutia tukio hilo.”