Supastaa wa muziki barani Afrika kutoka pande za Nigeria, Davido amekuwa akianika uhusiano wake ya msanii mwenzake, Wizkid akidai kuwa kwa sasa wameshaachana na bifu na ni marafiki wa kawaida.
Kulingana na Davido, amesema kuwa kwa sasa hawana bifu tena baada ya kukaa chini na kumaliza tofauti zao ambapo kwa sasa Wizkid amekuwa akimpigia simu Davido kila wiki tangu apoteze mtoto wake David Ifeanyi Adeleke Jr, aliyefariki dunia Oktoba 31, 2022 baada ya kuzama kwenye bwawa la kuogelea nyumbani.
“Mimi na Wiz kwa miaka kadhaa sasa tumekuwa hatuko karibu, ni takribani miaka 12 tulikuwa hatuzungumzi mpaka hivi karibuni aliponiandikia ujumbe wa simu na mimi nikaona ni jambo la kheri.
“Ninaona mabadiliko makubwa kwenye tasnia ya muziki kwa sababu kila mmoja ameshuka chini ya mwenzake na kuwa mpole hasa kulingana na changamoto niliyopitia, sasa ananipigia simu kila wiki tangu mwanangu afariki,” Davido aliiambia Hot FM ya Marekani.
Katika mahojiano mengine na BBC, Davido aliwataka amashabiki zake kutogombana nan a mashabiki wa Wizkid kwa sababu wote kwa sasa ni marafiki badala yake wasapoti albam za wasanii hao ambazo zimetoka hivi karibuni, ‘Timeless‘ ya Davido na ‘More Love Less Ego‘ ya Wizkid.