Diamond apiga magoti kanisani na kuombewa mtoko wa pasaka.
Wakati waumini wa Kikristo duniani kote wakisherehekea Pasaka – kusulubishwa na kufufuka kwa Yesu Kristo, nchini Tanzania kulikuwa na tukio kubwa Zaidi la mtoko wa Pasaka ambalo liliandaliwa na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya habari ya Wasafi, Diamond Platnumz.
Japo yeye ni Muislamu kindakindaki, Platnumz alijitoa kwa hali na mali na kufanikisha mtoko huo mkubwa ambao katika historia ya muziki wa injili kwa mara ya kwanza aliwakutanisha kwenye jukwaa moja waimbaji wa muda mrefu wa injili Rose Muhando na Christina Shusho.
Katika picha na video ambazo zimesambazwa mitandaoni kutoka tukio hilo la usiku wa Jumapili ya Pasaka, msanii Diamond alifanya kitendo cha ajabu baada ya kukubali kupiga magoti mbele ya wachungaji ambao walimwekea mikono ya Baraka kwa maombi, wakimtakia mafanikio makubwa katika mishe zake, haswa tukio kubwa la kutotaka dini kumbagua kutoka kwa mtoko huo.
Mtoko huo wa pasaka ulifanyika katika ukumbi mmoja Milimani City na Platnumz anaonekana akiwa amenyenyekea mbele ya watumishi wa Mungu akifanyiwa maombi.
“Kila nchi, kila bara likasherehekee kazi anazozifanya… familia nyingi zinaishi kwa sababu ametambua mchango, hakuangalia dini wala kabila, ameangalia utu na uzalendo. Yesu unayembariki hakuna wa kumlaani, na kazi yake izidi kutambulika…” mchungaji mmoja alionekana aimuombea Diamond.
Msanii Diamond akizunguza baada ya maombi hayo alisema kwamba huo ndio ulikuwa mwanzo wa ushirikiano mzuri ambao analenga kuufanya baina ya Wakristo na Waislamu.
“Tuendee kushirikiana, nimeongea na kamati pale na huu ndio mwanzo tu. Tutaendela kushirikiana na kuunga mkono katika kila idara, si tuo kila mwaka lakini katika kila muda,” Platnunz alisema.