Bester, alidanganya kifo chake kwa usaidizi wa Magudumana kumficha alipotoroka jela, Mangaung, Mei mwaka jana.
Wawili hao wamekuwa mafichoni tangu picha zao kusambaa wakiwa wanafanya shopping J’burg, mapema mwaka huu.
Walinaswa mjini Arusha siku ya Jumatano iliyopita wakiwa na passport nyingi zenye majina tofauti tofauti.
Ingawa bado hajafunguliwa mashtaka rasmi, kulingana na polisi, atakabiliwa na mashtaka ya kusaidia na kusaidia kutoroka gerezani, mauaji, na udanganyifu.
Wakati akifikishwa mahakamani, Dk Nandipha aliunganishwa na baba yake mzazi, na wengine wanne akiwemo mfanyakazi aliyepewa kandarasi ya kufunga kamera za CCTV jela aliyokuwepo Bester.
Kesi dhidi ya Nandipha imeahirishwa hadi Aprili 17, 2023, na haijajulikana kama daktari huyo amebadilisha maelezo yake ya awali.