Msanii asiyeishiwa vituko mjini Gift Stanford 'Gigy Money' amesema kwa sasa anaye mpenzi wake ambaye ni bilionea lakini hamlelei mwanaye Mayra.
Aamesema, yeye anapambana kivake kwamba licha ya kuwa na mpenzi huyo mwenye hela, anajua namna ya kumchekecha na kujikuta akimhudumia mwanaye pamoja na mishe zake binafsi.
"Hanilelei mtoto kwanza na yeye ana watoto wawili, mimi mwenyewe ndio najua namsomeshaji na namlisha nini mwanangu. Baba yake anaishia kuongea naye tu kwa simu hivyo," alisema Gigy.
Gigy amesema, anamlipia ada mwanaye karibu Milioni tano kwa mwaka na hajawahi kufeli, analipa kila mwaka.