Aliyekuwa Mke wa Mchezaji Achraf Hakimi aitwaye Hiba Abouk baada ya kuachana na Mumewe huo March 27,2023 aliwasilisha kesi ya kudai talaka huku akitaka kugawiwa nusu ya mali za Hakimi.
Baada ya Mahakama kufanya tathimini za mali hizo ilibaini kuwa Hakimi hamiliki chochote kwani mali zake zote zimesajiliwa kwa majina ya Mama yake.
"Hana mali, magari, nguo kwa jina lake, nyumba, vito au hata wakati wowote na akitaka chochote huwa anaomba kwa Mama yake ambaye huwa anamnunulia" - Mahakama ilitoa taarifa hiyo.
Inakadiriwa Kuwa Hakimi ana Utajiri wa zaidi ya Tsh Bilioni 45 ila Mali zote zinamilikiwa na Mama yake, Bi Fatima.
Aidha, inadaiwa kuwa Hakimi alijuwa wazi kuwa Mke huyo atataka mali zake hivyo aliziamisha umiliki kuwa za Mama yake mapema, ili yakitokea haya awe salama.