Hakuna Ushindi Mdogo Dhidi ya Wydad - Jemedari

 


Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka EFM, Jemedaeri Said amewapa maua yao klabu ya Simba baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya mabingwa watetezi wa kombe la mabingwa Afrika, Wydad AC ya nchini Morocco.


Simba na Wydad watarudiana keshokutwa Ijumaa, kwenye mchezo wa pili wa robo fainali katika Dimba la Mohammed wa V nchini Morocco.


Hakuna ushidi dhidi ya Wydad kwenye robo fainali ambao ni Ushindi Mdogo, kila unaposhinda dhidi ya vilabu vya Afrika Kaskazini wewe ukiwa unatoka eneo jingine lolote la Afrika basi umepata ushindi mkubwa.


Sikutegemea Simba wafanye chochote zaidi ya walichofanya dhidi ya Mabingwa watetezi wa CAFCL. Tofauti ya ubora ni kubwa sana kati ya timu hizi mbili kuanzia mchezaji mmoja mmoja,vikosi na mabenchi ya ufundi.


Hii inatokana na nguvu za kiuchumi za vilabu hivi kuwa tofauti sana pia. Bajeti ya Wydad ni zaidi ya Mara 10 ya ile ambayo Simba na vilabu viingi vya Kusini mwa Jangwa la Sahara inazo au inaweza kumudu.


Kuna mengi ya kujifunza kutoka kwao kabla ya kushindana nao ile Toe-to-Toe, bado hatujapata huo uwezo. Kwahiyo ukiwafunga kamavile ni jambo kubwa sana.


Jana Robertinho na vijana wake walikuwa na mpango kazi mzuri kiwanjani ambao umewapa ushindi wa kihistoria na kuandika rekodi mpya.


Makosa kama ya Onyango na wengine unayategemea unapocheza na timu bora, kwakuwa kuna wakati wanakulazimisha kufanya makosa kutokana na ubora wao, uzuri hawakufanikiwa kumaliza game hapa Kwa-Mkapa bado kuna nafasi ya kupambana Mohamed V pale Casablanca.


Kuvuka kwenda nusu fainali haitegemei kabisa historia ya Simba kuwatoa Zamalek, bali ubora wa mbinu kwenye mchezo ujao.


Wachezaji wataamkaje na uwezo wao wa kufanya yale waliyokubaliana kiwanjani utakuaje. Job well done Mnyama, Kila la kheir mechi ijayo.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad