Ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu msanii @harmonize_tz atuonyeshe kwenye mitandao ya kijamii kuwa yuko Zanzibar kwaajili ya kushuti video ya baadhi ya nyimbo zake ,taarifa aliyoitoa #Harmonize leo ni kuwa amezuiwa na @baraza_la_sanaa la Zanzibar kufanya video Zanzibar katika mwezi huu mtukufu wa Ramdhan.
Katika video mbalimbali zinazosambaa mtandaoni zinamuonyesha @harmonize_tz akiomba radhi kwa wana Zanzibar kama kuna usumbufu wowote aliowasababishia huku akiweka wazi kuwa hakusikia tangazo kutoka serikali ya Zanzibar kuhusu katazo la kushuti video kwenye kipindi cha mwezi huu mtukufu wa Ramadhan japo anasema alikaribia kumaliza kuzishuti video hizo.