Hasara za REA zilisababishawa na uzembe’



Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

UKAGUZI wa Ufanisi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) ameimulika REA kuanzia mwaka 2015/2016 mpaka 2019/2020.

Ukaguzi huu umefanyika kwa maombi ya wafadhili; Shirika la Kimataifa la Maendeleo Sweden (Sida) kwamba Machi 2016, Tanzania na Sida waliingia mkataba wa ufadhili wa kutandaza umeme vijijini. Fedha zilitoka SEK milioni 600 (Sh bilioni 133).


Uzembe wa kuchelewa kupakua malighafi Bandari ya Dar es Salaam, ulisababisha REA watumie Sh milioni 775.76 kulipa tozo ya uchelewaji (demurrage charge), hivyo fedha za ufadhili zikatumika ndivyo sivyo kwa uzembe.

CAG amebaini kuwa transfoma zilizofungwa uwezo wake ni 50KV, wakati bajeti ilikuwa 100KV , hii inamaana kwamnba fedha za wafadhili zilipigwa cha juu.

Upembuzi yakinifu haukufanyika. Hata udongo haukupimwa. Nguzo zimewekwa pasipo vipimo. Pesa ya upembuzi yakinifu (feasibility study), imepigwa.

Wateja 51,425 tu kati ya 98,689 walioomba kuunganishiwa umeme, ndio wameungabishiwa, kiwango hicho ni sawa na asilimia 52.1.

CAG ameandika; “Nyaraka za Sida zinaonesha REA walitakiwa kusambaza umeme kwenye nyumba 86,000, hivyo kuhudumia watu 430,000 kupitia gridi ndogo (Green Min and Micro Grid). Wameishia nyumba 17,302, yaani asilimia 20,”.

Aidha, uzembe wa kutohuisha taarifa za utafiti wa mradi, ulisababisha REA kuingia gharama za ziada Sh milioni 160.

Kuna jumla ya Sh bilioni 5.94, ambazo REA wamekuwa wakizitenga kama bajeti ya matangazo na elimu lakini hakuna maelezo ya zilivyotumika.

Mwaka 2018/2019, REA walitengeneza bajeti ya kununua transfoma na kuunganishia wateja umeme Sh bilioni 254.8. CAG akagundua, gharama halisi ilikuwa Sh bilioni 117. Kwa hiyo kulikuwa na udanganyifu wa Sh bilioni 137.8. Ufisadi.

Lingine, REA wilitumia Sh milioni 125.57, kununua transfoma 12 zilizo chini ya kiwango.

Siasa zikaingia. Tozo ya umeme kwa mwezi ikapitishwa Sh 11,000. Serikali ikasema tozo Sh 1,000. Gharama za uendeshaji zikawa kubwa kuliko mapato. Umeme ukazima vijijini.

Sehemu kubwa, CAG ameeleza tatizo la uchelewaji. Miradi ambayo ilipaswa kukamilika mwaka 2019/2020, mpaka sasa bado.

Hayo yalitokea Waziri wa Nishati akiwa, Dk. Medard Kalemani, aliyempokea Simbachawene kutoka kwa Muhongo, Rais akiwa hayati Dk. John Mgufuli.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad