Hawa ndio wanawake hatari zaidi duniani



Hawa ni Baadhi ya Wanawake wanao daiwa kuwa ni Hatari zaidi Duniani.

1. Anna Chapman

Huyu alikuwa jasusi wa Urusi na kwa mujibu wa mfanyakazi wa zamani wa CIA H. Keith Melton, ikiwa Anna angepewa miezi sita zaidi kutekeleza kazi yake, angekuwa "jasusi hatari zaidi katika historia ya Marekani". Anna alikamatwa pamoja na wapelelezi wengine 9 ambao kazi yao ilikuwa kuingia ndani ya taasisi za hali ya juu za Marekani na kupeleka habari.

2. Kanali Fanette Umuraza

Huyu ni namba mbili wa Jeshi la Mapinduzi la Congo Lkini pia kundi ambalo linajiita M23 na Umuraza ana mikono mbalimbali katika uhalifu wa kivita. Uhalifu huo ni pamoja na kitu kibaya kama ubakaji, mauaji, na kuajiri watoto kwa lazima. 

 3.Enedina Arellano Felix

Huyu alikua bosi mkuu wa kampuni ya Tijuana Cartel mwaka wa 2008. DEA baadaye ilimtangaza kuwa mwanamke wa kwanza kwa uhalifu duniani. Chini ya Enedina Arellano Felix na mtoto wake Fernando Sanchez Arellano, shirika lao linazingatia zaidi utekaji nyara kuliko mauaji. 

4.Maria Licciardi

Huyu aliendesha shirika la uhalifu la Camorra huko Naples,Italia. na Alipokuwa mafichoni, Licciardi bado aliamuru mauaji na pia alishambulia kwa bomu ofisi ya mwendesha mashtaka. Maria Licciardi baadaye alikamatwa mwaka 2001. . 

5. Samantha Lewthwaite

Huyu anajulikana kama Mjane Mweupe alizaliwa Ireland Kaskazini na kukulia nje ya London. Anahusishwa na kupanga shambulio la bomu katika eneo la mapumziko la Kenya mwaka wa 2011. Lewthwaite anaripotiwa kuwarithisha watoto wake kuendeleza ugaidi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad