Jinsi Wachezaji wa Simba Walivyomlinda Kipa wao Mchanga Kiakili na Kimwili Mcheza wa Simba Yanga


Kila mchezaji wa Simba alikuwa anajaribu kumlinda @salimjuma731 kiakili na kimwili ili aendelee kuwepo kwenye mchezo. Utaona kila alipokuwa akifanya jambo zuri karibu wachezaji wote walikuwa wanaenda kumuonesha wapo pamoja nae na kile anachokifanya wanakithamini.”

“Ingetokea wanamfokea/kumkaripia pale alipofanya makosa inawezekana angehisi yupo golini lakini wachezaji wazoefu hawamuamini.”


“Lakini uwepo wa Ally Salim golini uliongeza umakini kwa wachezaji wengine kwa sababu wanatambua golikipa wao si mzoefu wa mechi za aina ile kwa hiyo jukumu lao ni kuhakikisha hafikiwi na purukushani nyingi na kama itatokea anafikiwa basi iwe hakuna namna ya kuzuia.”

“Mazingira ya aina hiyo ameshakutananayo Manyika Jr, Kabwili na jana ilikuwa kwa Ally Salim. Timu nzima inakuwa makini kwa sababu wanajua kuna mtu sio mzoefu wa mechi kubwa.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad