Kendrick Lamar Aivunja Rekodi Hii ya Drake


Kendrick Lamar ameivunja rekodi ya Drake, kwa kuwa rapper mwenye ziara ya muziki iliyotengeneza mkwanja mrefu zaidi.

Kwa mujibu wa Touring Data, Big Steppers ya K.Dot ndiyo ziara ambayo imetengeneza hela nyingi zaidi kwenye historia ya Hip Hop.

Ziara hiyo imetengeneza dola milioni 110.9 kutokea kwenye mauzo ya tickets 929,000 kupitia shows 73.

Hii inamuweka Kendrick Lamar juu ya Drake na Migos ambao walikuwa wanaishikilia rekodi hiyo tangu 2018 na ‘Aubrey & The Three Migos (Amigos) Tour.

Ziara zingine zinazotajwa kutengeneza mkwanja mwingi kwenye Hip Hop ni kama ifuatavyo:

Drake na Future - Summer Sixteen

Kanye West na JAY-Z - Watch the Throne,

Kendrick Lamar - DAMN

Travis Scott - Astroworld

The Big Steppers Tour ilianza Julai 2022 kufuatia ujio wa albamu ya tano ya Kendrick Mr. Morale & The Big Steppers. Ziara hiyo ilimalizika mwezi Septemba mwaka 2022.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad