Kikosi cha Simba vs Wydad AC Mechi ya Leo 22 April Kwa Mkapa

Kikosi cha Simba vs Wydad AC Mechi ya Leo 22 April Kwa Mkapa


Kikosi cha Simba vs Wydad AC Mechi ya Leo 22 April Kwa Mkapa

Ally Salim

Shomari Kapombe

Joash Onyango

Henock Inonga

Mohamed Hussein

Mzamiru Yassin

Sadio Kanoute

Kibu Denis

Said Ntibazonkiza

Clatous Chama

Jean Baleke


Mchambuzi maarufu wa masuala ya soka nchini, Ramadhani Mbwaduke amesema kuwa Simba SC wanayo nafasi ya kushinda katika mchezo wao wa kwanza wa robo fainali ya Kombe la Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad AC.

Mbwaduke amesema kuwa hayo yanawezekana iwapo kocha wa Simba SC, Robertinho atafanya homework yake vizuri kwa Wydad kwani mbinu wanayotumia ni kama anayotumia Kocha Nabi wa Yanga ambaye wikiendi iliyopita Simba walimfunga bao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Wydad ambao Simba wanakwenda kukutana nao, mfumo wao wa jumla ni 4-2-3-1, huu ndio mfumo anaopenda kuutumia hata Kocha Nabi wa Yanga hata kwenye dabi alipanga hivyo, kwa mfumo huo, kipa ndio anaanzia kujenga mashambulizi.

“Simba SC wanapokwenda kucheza na Wydad, asilimia kubwa wanakwenda kuboresha kile walichokifanya kwa Yanga. Simba wakabie juu, kuwanyima pumzi mabeki wao. Angalizo kwa Simba ni kwamba, wachezaji wengi wa Wydad ni wazoefu lakini umri umeenda kidogo lakini haimaanishi hawana uwezo.

“Viungo wa kati wa Wydad umri wao ni mkubwa, kwa hiyo Simba wanaweza kucheza na hilo eneo waka-press mipira kwa kasi, wanaweza kuambulia kitu.

“Wakichukua kopi ya walichokifanya kwa Yanga mfano Simba wakapata mabao mawili, wapaki basi kisha wanapiga counter attack mkienda kwao mnashikilia bomba. Simba wanaweza kutumia pia mchezo wa kwanza wa Wydad dhidi ya JS Karbilie ambapo Wydad alifungwa bao moja, kuna kitu watajifunza udhaifu wa hawa Waarabu wakiwa ugenini.

“Unapocheza na Wydad ambaye yupo nafasi ya pili kwenye ubora CAF, Simba nafasi ya nane, lazima Simba amheshimu Wydad, wale wanamzidi kila kitu kuanzia uwekezaji, mafanikio lakini kwenye soka lolote linaweza kutokea, uwezo huo wanao, wakichukulia poa itakuwa shida,” amesema Bwaduke.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad