Kiroho Safi! Aishi Manula Ampongeza Ally Salimu Kwa Kudaka Mishale ya Yanga

 


Golikipa namba moja wa Simba SC,Aishi Manula,amempongeza golikipa namba tatu wa timu hiyo kwa kuweza kuhimili mechi ya dabi na kuondoka na clean sheet.


Ally aliaminiwa kuanza leo na Kocha wa timu hiyo, Roberto Oliveira 'Robetinho' katika mechi ya dabi dhidi ya Yanga SC, na wekundu hao wa Msimbazi kuondoka na ushindi wa goli 2-0.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Aishi aliondoka maneno haya kama kumpongeza kijana huyo ambaye ni mara yake ya kwanza kuaminiwa katika mechi kubwa ya dabi


"No Aishi Manura, No Beno Kakolanya, no problem," aliandika Aishi.


Simba wamecheza mchezo huo wa dabi wa 26 katika Ligi Kuu ya NBC na kufanikiwa kufikia alama 63 nyuma ya Yanga wanaoongoza Ligi wakiwa na alama 68. Zimesalia mechi nne kwa kila timu kukamilisha msimu wa Ligi Kuu 2022/23.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad