Ni ngumu kutafuta wema wa huyu jamaa kwenye hili, hata kama alikuwa na sababu zake au kuna mambo yalikuwa yanaendelea nyuma ya pazia baina yao, ila kitendo cha kumrekodi mkeo akinywa sumu hadi anafariki huku watoto wenu wadogo wakishuhudia, dah! Ni ushetani wenye PhD.
Hata kama Mwanamke alikuwa na visirani kiasi gani, alimuudhi kiasi gani, alitishia kujiua mara ngapi, bado kulikuwa na room ya jamaa kuokoa uhai wa mke wake.
Wanasema la kuvunda halina ubani, hata ulipige aina gani ya marashi bado litanuka tu, baada ya miezi 8, inakuja julikana mwana ndiye aliyerekodi tukio zima la kujiua kwa mkewe, wakati alijiliza sana mitandaoni baada ya kifo cha mkewe.
Sipati picha chuki ya watoto kwa baba yao, wanaweza wakawa sawa kwa sasa sababu ya umri mdogo, ila wakifika utu uzima na mwamba bado yupo hai, na sekeseke ndio hili limeanza upya.
Jamaa anapaswa kuwa ndani kutoa maelezo zaidi ya tukio hili, hata akiwa nje, sidhani ataishije na jamii hii ya teknolojia.