Mahakama Nchini #GuineaBissau imetoa adhabu hiyo baada ya kubaini kuwa Madaktari walihusika na matendo hayo dhidi ya M'Mah Sylla, aliyebakwa akiwa Hospitali na kuhamishiwa kutibiwa Nchini Tunisia Mwaka 2021
Waliohukumiwa ni Daniel na Patrice Lamah ambao wamepewa kifungo cha Miaka 15 jela na Daktari wa 3 ni, Celestin Millimouna ambaye alikimbia Nchi baada ya tukio hilo amehukumiwa kifungo cha Miaka 20 jela
Kwa mujibu Mashtaka, wote walipatikana na hatia ya kushambulia, kupiga risasi pamoja na kutoa Mimba huku Patrice Lamah na Millimouna wakikutwa pia na hatia ya Ubakaji.