Mange Kimambi Afunguka "Basata Wapuuzeni Wasanii Wote Wanaosema Hawataki tuzo"


Kutoka kwenye ukurasa wa Instgram wa Mwanaharakati wa Mitandaoni @mangekimambi_ Ameandika...

"Dear Basata, nimeona leo mmevamiwa sana. Huu hapa ushauri wangu kwenu ili

1. Wapuuzieni wasanii woote wanaosema hawataki kutajwa kwenye tuzo zenu. Hata huku marekani kuna wasanii huwa wanasusia tuzo ila hata msaniii asusie tuzo bado atakuwa nominated na kama kashinda bado atatangazwa kama mshindi na tuzo yake huwa inapokelewa na mtu. Hii ya kuruhusu msanii aseme hataki kutajwa then hamumtaji itafanya Tz kusiwe na music awards maana kila msanii ambae hatoshinda atasema hataki tena kutajwa.

2. Wekeni kamati inayoeleweka iwe unachagua nominees. Kamati iwe impartial kwa mfano, kamati iwe na watu kutoka radio zote, tv zote. Na sio watu wa radio/tv tu, kamati inaweza kuwa mpaka na wanasiasa na wasanii wa kuigiza etc. Kamati iwe na watu kama 100 hivi kutoka sehemu tofauti tofauti, ili mradi kamati iwe diverse. Kamati inakutana na kupiga kura nani awe nominated na nani awe mshindi.

3. Msiruhusu msanii kuleta kazi yake na kuchagua category. Kazi zao ni public na kila mtu anazijua. Wao wapige kazi watulie wasubiri kutajwa.

3. Muwe na msimamo.

Hakuna awards ambazo hazilalamikiwi duniani."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad