Helikopta za kijeshi za Marekani zagongana na kuanguka Alaska Photos/George Calin/via REUTERS
Nairobi – Wanajeshi watatu wafariki na mmoja kujeruhiwa baada ya Helikopta waliokua wanasafiria kugongana na kuanguka karibia Healy,Alaska.
Helikopta za kijeshi za marekani zimegongana na kuanguka katika eneo la Healy ,Alaska wakati zikirejea kutoka kwa mafunzo .Amesema msemaji wa jeshi la marekani John Pennell.Kulingana na taarifa ni kuwa aliyejeruhiwa amefikishwa hospitalini .
Kila Helikopta aina ya AH-64 ilikua imebeba wanajeshi wawili kabla ya ajali hiyo kutokea.Jeshi hilo limesema chanzo cha ajali hiyo kinachunguzwa na taarifa zaidi zitatolewa pindi zitakapopatikana.
Hii ni ajali ya pili kuhusisha helikopta za kijeshi huko Alaska mwaka huu. Mnamo Februari, wanajeshi wawili walijeruhiwa wakati helikopta ya Apache ilipobingiria baada ya kupaa kutoka Talkeetna.
Mnamo Machi, wanajeshi tisa waliuawa wakati helikopta mbili za Jeshi la Marekani za Black Hawk za kuwahamisha afya zilipoanguka wakati wa mazoezi ya kawaida ya usiku, kilomita 48 (maili 30) kaskazini mashariki mwa Fort Campbell, Kentucky.