Maskini...Nini Kimemkuta Rosa Ree ? Aweka Video Akilia na Kuandika Haya


IM NOT FINE! Mara nyingi naulizwa “How are you?” Nasema “I’m fine” kusema tu ila sio kumaanisha. But now I admit IM NOT FINE!

Napitia mambo mazito mpaka naona giza tu. Inaumiza kwamba haijalishi ninachopitia lazima niendelee kuonyesha furaha kwenye mitandao kana kwamba niko sawa. Kila siku napaswa niendelee kutimiza jukumu la kuwaburudisha, kupromote album, kutoa ngoma mpya, kurecord, kushoot videos na kuinspire jamii. SIKO SAWA! NAUMIA! NAPITIA MAMBO MAZITO KUYABEBA! NAONA KIZA! NAJIULIZA MASWALI MAJIBU SIPATI! Na kwa wakati huu Nani nimuendee? Mmepata burudani kutoka kwangu ila nikiwa sipo sawa mnanisaidiaje?? Nawaza sometimes kuwa wazi na haya ninayoyapitia ila nashindwa maana najua wengine watanicheka, wengine watanisema, wengine watanitenga na wengine hawatajali kabisa. Nyinyi si ndio familia yangu, sasa wapi niende?

Nikizungumza ninayoyapitia yatakua tu headlines ya story kwenye page za udaku? Nitapigiwa simu kufanya interviews ili media zipate story? Yani maisha yangu ni sinema tu kwa ajili ya kuwapa watu views? Na hisia zangu je? Na hata nikiwa sipo maisha si yataendelea tu????…..Honestly, IM NOT FINE!

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad