Mayele aipeleka Yanga nusu fainali ASFC




Dar es Salaam. Bao pekee la mshambuliaji Fiston Mayele limetosha kuipeleka Yanga katika hatua ya nusu fainali ya kombe la Shirikisho Azam baada ya kuivaa Geita Gold katika Uwanja wa Azam Complex.

Mayele alitumia dakika 13 tu kufunga bao hilo na kuonyesha wazi kukaa kwake benchi aliweza kuusoma vizuri mchezo.

Mayele aliingia dakika ya 45 kipindi cha pili akichukua nafasi ya Clement Mzize na dakika ya 58 alifunga bao akitumia vizuri pasi ya Tuisila Kisinda.

Katika kipindi cha kwanza mchezo ulionekana kuwa mgumu huku kila mmoja akionyesha nia ya kuhitaji bao lakini hakuna aliyefanikiwa kufungua mlango wa mwenzie hadi wanaenda mapumziko.


Dakika 45 za kipindi cha kwanza mwamuzi Abdul Wajihi kutoka Tanga alitoa kadi tatu za njano tatu moja ikiwa upande wa Yanga na mbili Geita Gold.

Mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize alikuwa wa kwanza kuonyeshewa kadi ya kwanza ya mchezo dakika ya 37 baada ya kumchezea madhambi beki wa Geita, George Wawa.

Kadi ya pili ya njano ilikuwa dakika ya 40 kwa beki Geofrey Raphael baada ya kumfanyia madhambi Kennedy Musonda na ya tatu akionyeshwa Joffrey Manyasi.


Yanga ilifanya mabadiliko ikiwaingiza Stephan Aziz Ki, Fiston Mayele, Jesus Moloko na Bernard Morrison huku wakitoka Clement Mzize, Yannick Bangala, Kennedy Musonda na Tuisila Kisinda.

Upande wa Geita aliingia Dany Lyanga, Bakari Rashid, Amosi Kadikilo na Offen Chilla wakichukua nafasi ya Deusdedit Okoyo, Abdulswamad Kassim, Edmund John na Elias Maguri.

Geita walilazimika kumaliza mchezo wakiwa pungufu baada ya kiungo wao Geofrey Manyasi kupewa kadi nyekundu ikiwa ni njano ya pili, mchezo huo ukitamatika na jumla ya kadi saba za njano kwa timu zote na nyekundu moja.

Yanga inatarajia kucheza na Singida Big Stars katika nusu fainali ya Kombe la Azam huku Simba ikicheza dhidi ya Azam FC.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad