Mbunge wa Babati Vijijini, Daniel Sillo Achukua Nafasi ya Zungu Bungeni



Dodoma. Mbunge wa Babati Vijijini, Daniel Sillo amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa bunge ili kurithi kiti kilichoachwa wazi na Mussa Zungu baada ya kuchaguliwa kuwa Naibu Spika.

Leo Jumanne April 4,2023 Bunge kwa kauli moja limewapitisha Najma Giga (Viti Maalum), David Kihenzile (Mufindi Kusini) na Daniel Sillo kuwa Wenyeviti wa Bunge baada ya kupitishwa na Kamati ya Uongozi.

Hata hivyo Wabunge Kihenzile na Najma walikuwa Wenyeviti wa Bunge kabla ya leo ambapo kipindi hicho walikuwa watatu akiwepo Mussa Zungu ambaye sasa ni Naibu Spika.

Sifa za Mbunge kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bunge ni lazima awe Mwenyekiti au Makamu wa Kamati mojawapo za Bunge kwa kuangalia pande za Muungano.

Zungu alichaguliwa kuwa Naibu Spika akichukua nafasi ya Dk Tulia Akson ambaye alichaguliwa kuwa Spika akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Job Ndugai ambaye alijuzulu wadhifa huo mapema mwaka 2022.

Kanuni za Bunge zinaelekeza kuwa, Kamati ya Uongozi itapeleka majina yasiyozidi sita mbele ya Bunge ili watatu wachaguliwe kwa nafasi hiyo suala la Muungano likizingatiwa.

Kwa mujibu wa Spika, mapema jana Kamati ya Uongozi ilipitisha majina matatu ambayo yamepelekwa mbele ya Bunge na kwamba kanuni zinasema kuwa ikiwa idadi ya wagombea itakuwa sawa na nafasi zinazoombwa, wabunge watapiga kura ya pamoja kwa kuwathibitisha.

Wabunge hao wamepewa nafasi ya kushukuru ambapo kila mmoja ameomba ushirikiano kutoka kwa wabunge na wao kusema watafanya kazi kwa bidii na maarifa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad