Jeshi la Polisi nchini Kenya limemkamata Mchungaji mashuhuri nchini humo, Ezekiel Ombok Odero wa kanisa la New Life Prayer Centre lililopo mtaa wa Mavueni mjini Kilifi kwa tuhuma za mauaji. Ofisi ya DCI imeeleza kuwa Pastor Ezekiel ametajwa kuhusika na vifo vya watu 98 vilivyotokea katika kanisa la Good News International Ministry la Mchungaji Paul Mackenzie.
Pia anatuhumiwa kwa vifo vingine vilivyotokea katika kanisa lake kwa kushawishi waumini wake kutorosha ndugu zao wagonjwa hospitalini na kwenda kuwaombea.
Katika tuhuma za kwanza, Pastor Ezekiel ametajwa kuwa mshirika wa Mchungaji Paul Mackenzie kwa kufanya mahubiri potofu ya kushawishi watu kufunga hadi kufa. Hapo jana mmoja wa wachungaji wasaidizi wa Ezekiel alisema kuwa Mchungaji Mackenzie alikua anafadhiliwa na Pastor Ezekiel na kwamba walikua na ushirika.
Akitoa maelezo yake mbele ya ofisi ya DCI, Mchungaji huyo ambaye polisi wamezuia kutaja jina lake, amesema Mchungaji Mackenzie alikua akilazimisha watu kufunga hadi kufa, na walipokufa Pastor Ezekiel alienda usiku wa manane kuchukua baadhi ya viungo vyao kabla ya kuzikwa usiku huohuo. Baadhi ya maiti zilizofukuliwa zimekutwa bila viungo kama sehemu za siri, ulimi, figo, ini, moyo etc.
Akaunti za benki za Mchungaji Mackenzie zimekutwa na ukwasi wa KSH Milioni 315, sawa na TZS Bilioni 5.5 ambazo ofisi ya DCI inashuku kwamba huenda zimetokana na biashara haramu ya viungo vya binadamu.!