Memba wa P Square afunguka" Nilitabiri Wizkid atakuja kuutawala huu Muziki

 


Mwimbaji wa Kundi la P-Square (Peter Okoye) maarufu kama Mr. P ameanika wazi jinsi alivyowahi kutabiri Wizkid atakuja kuwa msanii mkubwa na kutawala kiwanda cha muziki.


Kwenye mahojiano yake mapya na Podcast ya 77, Peter alitukumbusha miaka kadhaa nyuma ambapo alikutana na Wizkid akiwa anajitafuta kutoboa kwenye Muziki na kumtabirua makubwa.


“Sisi [P-Square] hatujawahi kuwa wasanii ambao tunachukulia poa mtu yeyote. Kama unakumbuka, kuna video iliwahi kusambaa sana ambayo ilikuwa ni tamasha letu na Wizkid alikuwa kama mtangulizi kwenye show hiyo.


Waandishi wa habari walikuwa wakituhoji sisi tu, tukasema hapana, kwanini msimfuate na yule [Wizkid] mkamfanyie interview? Nikawaambia huyu atakuja kuwa msanii mkubwa kesho.” Amesema Peter Okoye.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad