Mfanyakazi wa Benki Awaua Wafanyakazi Wenzake Watano Kwa Kuwapiga Risasi



Mfanyakazi wa Benki ya Old City Bank iliyopo Louisville, Kentucky nchini Marekani amewaua kwa kuwapiga risasi wafanyakazi wenzake watano wa benki hiyo huku wengine 9 wakijeruhiwa ambapo alikuwa akijirekodi na kurusha tukio zima mubashara kupitia akaunti yake ya Instagram.

Aliyefanya tukio hilo, anatajwa kuwa ni Connor Sturgeon (25) ambaye siku chache zilizopita, alipewa taarifa kwamba atafukuzwa kazi.

Polisi wameeleza kuwa mtuhumiwa alikuwa akitumia bunduki aina ya AR-15-style ambapo polisi walifika haraka eneo la tukio na kujaribu kumdhibiti lakini ikashindikana ndipo walipoamua kumpiga risasi na kumuua.

Kampuni ya Meta inayomiliki Instagram, imeifuta video ya tukio hilo, muda mfupi baadaye.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad