Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Jenista Mhagama kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) akichukua nafasi ya George Simbachawene
Kabla ya Uteuzi huo Mhagama alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Aidha Rais Samia Suluhu Hassan amemteua George Simbachawene kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora akichukua nafasi ya Jenista Mhagama ambaye sasa ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)