Mr Blue "Siwezi kuongeza mke Nimepata Mke Sahihi"



Nimepata mke sahihi siwezi kumuongezea mke mwenzie japo dini yangu inaruhusu - Mr.Blue.


Mr. Blue na mke wake huyo Waheeda Sylvester wamekuwa pamoja kwa takribani miaka 14 sasa tangu wakutane kwa mara ya kwanza katika klabu ya usiku ila Mr. Blue anasema kamwe hajafikiria na wala hatakuja kumuongezea mke mwenzie japokuwa dini yake inaruhusu, Mr.Blue anaeleza kwamba Waheeda ni mke bora na sahihi kwake na kwa watoto wao hahitaji kuanza kuleta migogoro katika familia yake.


Wawili hao wana miaka 8 tangu wafunge ndoa ukiacha miaka mingine takribani sita ya mahusiano ya kawaida, na kabla ya Waheeda Mr.Blue aliwahi kuwa katika mahusiano na wasichana kadhaa maarufu na wasio maarufu ila walishindwana Mr.Blue aliwahi kueleza kuwa walipokutana klabu na Waheeda kwa mara ya kwanza alimchukulia poa kama ilivyo mitazamo ya watu wengi kuwa mahusiano ya kukutana sehemu za starehe hayadumu na huwezi pata mke bora au mume bora huko ila ikawa tofauti.


Blue alieleza kwamba baada ya kupata mtoto wao wa kwanza alijiingiza katika utumiaji wa mihadarati na hivyo kuiweka afya yake na kazi zake za muziki katika uelekeo wa kuporomoka ila Waheeda hakutaka kumuacha Blue bali alihakikisha anamsaidia ikiwemo kumshauri aachane na kampani mbaya ya marafiki wanaotumia mihadarati kwani mwisho wake hautokuwa mzuri kwake na hilo likafanikiwa Kabla hawajakutana na kuoana.


Waheeda aliwahi kushiriki Miss Tanzania 2008 akaingia top 10 na baadaye akawa video vixen katika baadhi ya kazi za wasanii wa Bongofleva na kupamba kurasa za baadhi ya majarida maarufu ingawa hakuwahi kukumbwa na skeno yoyote chafu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad