Msemaji wa Polisi wa Tanzania Afunguka Kuhusu Thabo Bester na Mpenzi Wake Nandipha Waliokamatwa Tanzania

 


Mhalifu maarufu wa Afrika kusini Thabo Bester na mpenzi wake Dr Nandipha Magudumana hawataendelea na kesi yoyote katika mahakama ya Tanzania, watashtakiwa katika mahakama za Afrika Kusini.


Msemaji wa Polisi wa Tanzania, David Misime ameiambia BBC kuwa Bester na mpenzi wake huyo waliingia nchini kinyume cha sheria, lakini kwa mujibu wa sheria za kimataifa watafata utaratibu wa kuwarudisha Afrika kusini ili waendelee na mashtaka yao.


“Baada ya polisi wetu kupata taarifa zake na anayedaiwa kuwa mpenzi wake Dk Nandipha. Walikamatwa na bado wapo kizuizini. Tunakamilisha taratibu za kisheria kati ya nchi hizo mbili na tutamkabidhi kwa maafisa wa Afrika Kusini.


Siku ya Jumamosi Polisi walithibitisha kukamatwa kwa Thabo Bester, mpenzi wake Dk. Nandipha Magudumana, na Zakaria Alberto huko Arusha, Kaskazini mwa Tanzania.


Bester ambaye anajulikana kama "mbakaji wa Facebook" kwa kutumia mtandao wa kijamii kuwarubuni waathiriwa wake.


Alipatikana na hatia mwaka wa 2012 kwa kumbaka na kumuua mpenziwe mwanamitindo Nomfundo Tyhulu. Mwaka mmoja mapema, alipatikana na hatia ya kubaka na kuwaibia wanawake wengine wawili.


Alifanikiwa kutoroka gerezani na kuaminisha mamlaka za Afrika kusini kuwa alijiua kwa moto katika chumba chake cha gereza.


Wakati huo huo, Askari wa gereza aliyesimamishwa kazi na baba yake mpenzi wa Thabo Bester wanakabiliwa na msururu wa mashtaka yakiwemo mauaji, uchomaji moto na kusaidia kutoroka kwa Thabo Bester.


Kulingana na stakabadhi za mahakama, watu hao wawili wanadaiwa kumuua kimakusudi mtu asiyejulikana Machi mwaka jana.


Kesi yao imeahirishwa hadi Aprili 17 kwa uwezekano wa maombi ya dhamana, Wamewekwa rumande ya polisi.


Kampuni ya ulinzi inayomilikiwa na Uingereza ya G4s ilikuwa ikiendesha gereza alimofungiwa Bester. Tangu wakati huo imechukuliwa na maafisa wa magereza ya Afrika Kusini kufuatia kashfa yake ya kutoroka

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad