Mtangazaji Maarufu wa CNN ambaye pia ni shoga Apata Uraia wa Marekani



Mtangazaji maarufu wa CNN ambaye pia ni shoga, Richard Quest amefichua fahari yake ya kuchukua uraia wa Marekani mbele ya mpenzi wake wa kiume, Chris.

Mwanahabari huyo alishiriki habari hiyo ya kusisimua kwenye Twitter.

“Nilikuwa raia rasmi wa Marekani jana, nina fahari kubwa kuidhinishwa kama raia wan chi hii mbele ya mpenzi wangu Chris. Mimi sasa nina uraia pacha wa Uingereza na Marekani,” Quest alisema.

Quest, raia wa Uingereza, mnamo 2020 alifichua kuwa alikuwa amefunga pingu za maisha na mpenzi wake Chris Pepesterny.

Kupitia chapisho kwenye mtandao wa kijamii kipindi hicho, Quest, ambaye wote walikuwa wakitabasamu na Chris, alisema ilikuwa siku ya furaha zaidi maishani mwao.

"Tulisema 'I DO' wikendi. Siku ya furaha zaidi maishani mwetu,” aliandika.


Wawili hao awali walikuwa wamepanga kufunga ndoa Machi mwaka huu jijini London lakini ikabidi waahirishe.

Kulingana na sheria ya Marekani, mtu anahitimu kuwa raia aliyeidhinishwa ikiwa una umri wa angalau miaka 18 na umekuwa mkazi wa kudumu kwa angalau miaka 5 (au miaka 3 ikiwa umeolewa na raia wa Marekani) na kutimiza masharti mengine yote ya kustahiki. mahitaji.

Marekani hivi karibuni imekuwa ikikosoa Kenya, Uganda na nchi nyingine za Afrika ambazo hazikubali ndoa za jinsia moja.


Meg Whitman, Balozi wa Marekani nchini Kenya alisema pamoja na kwamba nchi yake inaheshimu sheria za Kenya, inazichukulia nchi ambazo hazikubali LGBTQ kama kukandamiza haki za watu hao.

Nchini Tanzania mapema wiki hii, munge mmoja aliwasilisha hoja akitaka wabunge waanze kufanyiwa vipimo vya afya kubaini wale "wanaoshughulikiwa" katika suala la tendo la ndoa baina ya watu wenye jinsia moja.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad