Mtangazaji mkongwe wa TV nchini Marekani, Jerry Springer Afariki Dunia


Mtangazaji mkongwe wa TV nchini Marekani, Jerry Springer aliyejipatia umaarufu kwa talk show yake pendwa na iliyokuwa na utata mwingi amefariki dunia. Alikuwa na umri wa miaka 79.

Springer amefariki Alhamis hii nyumbani kwake Chicago baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Kipindi chake, Jerry Springer Show kilichoanzishwa mwaka 1991 kilikuwa maarufu mno kiasi kwamba mwaka 1998 kilikizidi kipindi cha The Oprah Winfrey Show kwa kuwa na watazamaji wengi, kikivutia watu milioni 12.

Ameacha mjane, Micki Velton aliyefunga naye ndoa tangu 1973 na mtoto mmoja wa kike, Katie.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad