Mtumishi GGML aliyeuawa kikatili ameacha mtoto
Mwili wa mfanyakazi wa mgodi wa dhahabu wa GGML Milembe Selemani (43), aliyefariki dunia tarehe 26 ya mwezi huu kwa kukatwakatwa viungo vya mwili wake umeagwa nyumbani kwake katika Kijiji cha Sanjo, Kata ya Usagara wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
Sopspeter Kahano ambae ni shemeji yake marehemu Milemba mbali na kumsomesha marehemu anaeleza namna alivyomfahamu hadi alipoajiriwa katika mgodi wa GGML, na kwamba aliolewa japo ndoa yake ilivunjika na ameacha mtoto mmoja wa kike
"Milembe namfahamu nimemkuza nimemlea katika familia yetu alikuwa ni ambaye anajitoa sana na alikuwa na mchango mkubwa sana kwenye familia, kwahiyo tumempoteza mtu ambae ni muhimu sana kwenye familia aliwahi kuolewa akabahatika kupata mtoto mmoja wa kike na baada ya hapo waliachana kila mmoja akawa anaishi kivyake" amesema Kahano
Dotto Gabriel ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nyashimba Kijiji cha Sanjo, Kata ya Usagara anaeleza namna marehemu Milembe alivyokuwa anashiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii katika kitongoji hicho, "Alikuwa anashiriki vizuri tu kwenye kazi za jamii na alikuwa hana shida yoyote na jamii hata kwangu mimi kama kiongozi niliposikia kifo chake nilipokea kwa masikitiko na mshtuko kwa sababu sikutegemea kwanza kwamba haya yataweza kumkuta,"